International Student Office

Page address: http://www.mnsu.edu/iso/message/swahili.html

MSU > ISO > Director's Msg

[ English | Spanish | French | Russian | Swahili | Chinese | Japanese | Korean ]

Ujumbe Wa Thomas


Thomas GjersvigTunayo furaha kutokana na nia yako ya kupata msaada wa ofisi yetu na Chuo Kikuu cha Jimbo la Minnesota, Mankato. ISO, kama tunavyopenda kutambulika, inahudumia wanafunzi wa Kimataifa wapatao 600 kutoka zaidi ya nchi 50. Ofisi inapokubali maombi ya kujiunga na chuo husika, fomu zake huletwa kwetu kwa ajili ya kushughulikia taratibu za uhamiaji. Mwanafunzi aliyekubaliwa kujiunga na chuo hutumiwa, kutoka kwetu, Fomu I-20 au DS-2019, taarifa za kimataifa, maombi ya bwalo la kuishi na ile ya chanjo. Kadhalika ISO huwakumbusha Wanafunzi wa Kimataifa mara kwa mara kununua bima za afya kabla ya kusajiliwa kwa masomo. Tunakumbusha fomu hizi na bima kila mara kwani ni muhimu sana kwa kila Mwanafunzi wa Kimataifa kwa sababu ni matakwa ya sheria za Marekani kabla ya kupatiwa kibali cha kuishi kabla ya kuingia nchini.

Si hayo tu ambayo ISO inafanya. Hivi sasa tunasimamia shughuli zote za Chama cha Wanafunzi (ISA) ambacho kinahudumia Wanafunzi wote wa Kimataifa kwa mahitaji yao yote yanayotambuliwa na Chuo. ISA pia hushughulika na michezo, sherehe na miongozo kwa Wanafunzi. Hivyo kujiunga na ISA hutoa fursa ya kushiriki kwenye Serikali ya Chuo, kutoa mihadhara darasani, kushiriki majopo ya kimataifa na ndani ya nchi. ISO inasimama kama mhimili wa ISA ili Wanafunzi wa Kimataifa chuoni hapa waweze kupata uzoefu wa hali ya juu kutokana na elimu wanayoipata hapa Marekani.

Iwapo bado utakuwa unahitaji maelezo zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi:

Simu: 507-389-1281 (V) or 800-627-3529 (MRS/TTY)
Fax: 507-389-6225
Barua Pepe: iso@mnsu.edu

Wako,

Thomas C. Gjersvig, Director
International Student Office
219B Centennial Student Union
Minnesota State University
Mankato, MN 56001