Ofisi ya Wanafunzi wa Kimataifa (ISO) inasaidia kutoa huduma yenye lengo la kuwasaidia Wanafunzi wa Kimataifa kimasomo, mahitaji ya binafsi, ya kifedha na ya uhamiaji kwenye nyanja za elimu na fursa mbalimbali za maisha kwa Wanafunzi hao kutoka nchi nyingine.
ISO inatoa uzoefu na mahusiano ya Kimataifa kwa Wanafunzi wa MSU, kitivo cha elimu na jumuia ya Mankato. ISO imedhamiria kuinua kiwango cha uelewa wa Kimataifa na umuhimu wa kupambanua nyanja mbalimbali za maisha, utamaduni na elimu duniani kote.